TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania, Dr. Benson O. Ndiege amefuta jumla ya Vyama vya Ushirika 3,317 kwa kushindwa kutimiza masharti ya Usajili wa Vyama hivyo. Tangazo la kufuta kwa Vyama vya Ushirika hivyo limetolewa katika Gazeti la Serikali Na ISSN 0856 - 0323 Toleo Na.30 lilitolewa Tarehe 24/07/2020.